Leo january 20 ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya mfanya biashara maarufu wa nguo jijini Dar es Salaam Chidi Mapenzi ambaye ndiye mume wa mwanadada muigizaji maarufu Shamsa Ford.
Kama ilivyo kawaida na desturi ya watu wengi katika kusherehekea maadhimisho ya siku zao za kuzaliwa ndivyo vivyo hivyo ilikuwa kwa mastaa hao kwa kuamua kujumuika na familia usiku wa jana na kukata keki na vitu kama hivyo.
Katika mtandao wa Instagram mwanadada Shamsa Ford alidindisha ujumbe mzito kama caption kwenye post ya video ambayo ilionyesha familia hiyo ikikata keki katika tukio hilo la birthday.
Ujumbe ambao ulidhihirisha furaha ya mwanadada huyo Shamsa Ford katika maisha yake ya ndio na kuonyesha dhahiri kuwa hajutii maamuzi yake ya kuolewa na mfanya biashara huyo.
Ujumbe ambao ulisomeka kama “Kuna watu wakiingia kwenye maisha yako, hauwezi kujuta badala yake unaongezeka nakuwa BORA. Namshukuru MUNGU kwaajili yako, umekua rafiki, mshauri, mume bora,na msaada kwangu,nimekuwa bora kwenye maeneo MENGI. Am proud of you mume wangu kipenzi.NIMEPENDELEWA NA MUNGU kunipa mtu wa aina yako,nakupenda na nitakupenda siku zote,wewe ni Baraka kwangu.Happy birthday Baba shamsa. Mungu azidi kukulinda na kukufungulia mirango yote ya riziki. HAPPY BIRTHDAY MY ME”
0 comments:
Post a Comment