
Wiki
hii, habari kubwa nchini ilikuwa ni tukio la mfanyabiashara, Said Ally
kutobolewa macho, usiku katika maeneo ya Buguruni Sheli jijini Dar es
Salaam.
Jina
la ‘Scorpion’ – mtu aliyefanya unyama huo, limekuwa maarufu pia. Polisi
tayari wamemkamata na Jumatano hii alipandishwa kizimbani kusomewa
mashtaka mbalimbali yakiwemo kupora na kumjeruhi Said kwa kumchoma visu
mwilini na kumtoboa macho yake na kumpa upofu wa ukubwani.
SCORPION NI NANI?
Jina
lake halisi ni Salim H Njwete au Samjet. Unaweza ukawa umewahi kumuona
sehemu. Mwaka 2012, alikuwa mshindi wa shindano la Dume Challenge
lililowakutanisha vijana 20 wababe wa mazoezi na kazi ngumu. Salim
alijinyakulia kitita cha shilingi milioni 20.

Salim
Njwete aka Scorpion (Kushoto) akikabidhiwa mfano wa hundi kufuatia
kutangazwa mshindi wa shindano la Dume Challenge, December 2012
Ni
mwalimu wa karate na mbabe wa mapigano na ndio maana pindi
anamshambulia Said hakuna aliyethubutu kumsaidia kwasababu kila mtu
maeneo ya Buguruni anamhofia.
Ni
muigizaji wa filamu pia na kwa mujibu wa Walter, aliyekuwa mshiriki
mwenzake kwenye Dume Challenge, baada ya mashindano hayo Salim alitoa
filamu moja.
Walter
ameiambia Bongo5 kuwa Salim alikuwa mtu wa kawaida kabisa na ambaye
isingekuwa rahisi kumdhania angekuja kuwa mnyama kiasi hicho.

Walter
ambaye ni mwanamuziki na anayefanya kazi za ulinzi kupitia kampuni
yake, ni mmoja wa washiriki 20 walioshiriki kwenye shindano hilo
Walter anasema, Salim ni mjuzi wa mchanganyiko mapigano ya aina nyingi. Anadai aliposikia kuwa ndiye Scorpion, alishangaa mno.
“Lazima
nishangae kwasababu, ni kitu ambacho hujawasiliana na mtu kwa muda
mrefu kidogo halafu ghafla unakuja kusikia negative side ya mtu ambaye
mnafahamiana naye, na ambaye mlishirikiana naye kama wakati tupo kwenye
mashindano kule tulikuwa tunalala yaani kitanda hiki hapa na hiki hapa,”
Walter ameiambia Bongo5.

“Ni
mtu ambaye mmeshirikiana kitu fulani ambacho tayari kilishakuwa on
public na watu tayari washajua taswira yenu, sasa mtu anapokuja kufanya
kitu kama hicho, ina maana hata wewe mwenyewe unahisi taswira yako
inachukuliwa kama vile mshikaji,” ameongeza.
Walter
anasema baada ya kushinda milioni 20 kwenye shindano hilo, anachojua ni
kuwa Salim aliingia kwenye uigizaji wa filamu na pia alikuwa na mpango
wa kwenda kufanya kilimo. Anaeleza kuwa kwenye filamu, Salim alikuwa
chini ya Tuesday Kihangala maarufu kama Mr Chuzi.
“Aliamua
kuspend hizo hela zake katika movie na akabahatika kutoa movie moja
ambayo haikufanya vizuri katika industry,” anaeleza Walter. “Sasa maisha
baada ya hapo, sijui ndio akaamua kuspend hela zilizobaki kwenye kitu
gani, labda kwenye kilimo kwasababu wakati tulipokuwa naye kule kambini –
maake si unajua unamuuliza hizi hela unazifanyia nini, yeye alikuwa
amewaza kwenda kulima huko Morogoro.”
Walter
amesema washiriki wenzake wengine wa Dume Challenge wameshangazwa na
alichokifanya Salim. “Wako shocked yaani,” anasema. “Ni kitu ambacho
hakuna aliyetegemea kwamba jamaa alikuwa anaweza kufanya kitu kama
hicho.”
CHANZO: BONGO 5
0 comments:
Post a Comment