Posted by Williammalecela.com on Monday, October 10, 2016
 |
Seneta John McCain,
Miongoni mwa wanasiasa wa hivi punde zaidi ni pamoja na aliyekuwa
waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Condoleezza Rice, na
aliyegombea kiti cha urais nchini humo, Senator John McCain.
Lakini
Trump amesema kwamba hatajiondoa kutoka katika kinyang'anyiro cha
kuwania kiti hicho licha ya malalamishi kutoka kote duniani kutokana
na matamshi yake ya kuudhi kuwahusu wanawake, aliyo-yatoa mwaka 2005.
Zaidi
ya wanasiasa 24 wa chama chake cha Republican, sasa wamesema hadharani
kuwa hawamuungi mkono bilionea huyo na wanamtaka kumuachia mgombea
mwenza Mike Pence nafasi ya kuwania kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu
wa Marekani hapo mwezi Ujao.
Miongoni mwa wanaolaani matamshi hayo ya Trump ni pamoja na mkewe Trump- Melania. |
 |
Aliyekuwa waziri wa nchi za kigeni wa Marekani Condoleezza Rice
Amesema kuwa licha ya kuendelea kumuunga, analaani matamshi hayo mapotovu dhidi ya wanawake.
Spika
wa Bunge Paul Ryan, alizomewa na kushangiliwa kwa wakati mmoja, katika
mkutano mmoja wa kisaiasa baada ya kukataa kutumia jukwaa moja na Bwana
Trump. |
0 comments:
Post a Comment