SIKU chache baada ya kuripotiwa kupika na kupakua na staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma, Bond Suleiman ameibuka na kusema watoto wa mke huyo wa zamani wa Mbunge wa Donge, Sadifa Juma, hawakupenda mama yao aolewe na mtu mwingine zaidi yake.
Mbunge wa Donge, Sadifa Juma alipofunga ndoa na Wastara.
Akipiga
stori na Za Motomoto News, Bond alisema alipokuwa kwenye ndoa, watoto
hao walimfuata na kumwambia kuwa hawakufurahishwa mama yao kuolewa na
mtu mwingine kwa sababu ya mapenzi ya dhati aliyokuwa akimuonesha mama
yao enzi za uhusiano wao.
Wastara Juma.
“Upendo
wangu ndiyo uliomrudisha Wastara maana niliamua kubadilika na kuachana
na pombe kwa ajili yake, nawaomba wanawake wanaonisumbua kunitaka
kimapenzi waache kwani ninaye Wastara, mwanamke wa maisha yangu, siwezi
kumsaliti tena, ndani ya mwaka huu tutafunga ndoa,” alisema Bond ambaye
pia ni muigizaji.
0 comments:
Post a Comment