Mwanamitindo, Jokate Mwigelo kupitia kampuni yake ya kidoti ameandaa shindano la kusaka msusi bora alilolipa jina la msusi wao lengo ni kuwaamsha wasusi wasiokuwa na ofisi na kuwafanya wakitambue kipaji chao.
“Unajua siku moja
nilitafuta msusi nikaletewa nyumbani dada mmoja ambaye hana ofisi ambaye
alinisuka vizuri lakini nilipomuhoji anakazi gani inayompa kipato
hakuwa na kazi, ndipo niliona ipo haja ya kuwakuza wasusi wetu ikiwa
sehemu ya kutoa ajira na kuwafanya wajitambue,” alisema Jokate.
Jokate
alimtaja mshindi wa kwanza kuwa atapata nywele za Kidoti zenye gharama
ya shilingi milioni 1.5 Pesa shilingi laki tatu na Draya, wa pili
atapata nywele za gharama ya shilingi milioni 1.2 na laki mbili na Draya
na wa tatu atapata milioni moja na laki mbili na nusu pamoja na draya.
Washindi
watatafutwa kila wilaya ya ambapo kutakuwa na fomu za kujaza ili
kuwatambua vema na wanaohusika ni wale tu wasiokuwa na ofisi.
0 comments:
Post a Comment