
- Awataka wakulima kuungana na kuacha migogoro
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Leo ametembelea kiwanda cha chai cha WAKULIMA ltd na kufanya kikao na wadau wa chai wilaya YA Rungwe na kupokea kilio cha wakulima wadogo wa chai ambao ni wabia wa kiwanda cha chai cha WATCo kueleza
kuwa kiwanda chao kupata hasara kutokana na kampuni YA METL kununua chai kwa baadhi YA wakulima wakati hawana leseni hiyo na hivyo kumuomba Mkuu wa Mkoa kuingilia kati

Kampuni ya METL imekiri kuwa leseni yake ni YA kulima chai ktk mashamba yao na kusindika ktk viwanda chao
Kutokana na kiwanda cha wakulima wadogo kukosa chai kutokana na kugombania chai toka kwa wakulima kumepelekea kiwanda hicho kukosa malighafi 

Kutokana na malalamiko hayo na kutokana na kampuni ya METL kukosa leseni YA kununua chai hiyo amesitisha rasmi kampuni hiyo kununua chai na watumie leseni yao kulima chai ktk mashamba yao na kusindika chai ktk kiwanda chake
Kuendelea kununua chai kampuni ya METL imepunguza kulima na kutunza mashamba yake na ni kinyume na
makubaliano wakati wananunua kiwanda na mashamba hayo

Aidha amewataka wakulima kuungana na kuwa na nguvu YA pamoja badala YA kuendekeza misuguano isiyo na lazima



0 comments:
Post a Comment