

Hayo ameyasema leo wakati wa kikao cha wazi cha kusikiliza kero za wananchi na idadi kubwa YA malalamiko ni wananchi kulalamikia fidia, ucheleweshaji wa hati na kugawiwa kiwanja kimoja kwa watu zaidi YA mmoja

Kutokana na hali hiyo Mkuu wa mkoa amemwagiza mkurugenzi wa jiji na Mkuu wa idara ya ardhi KUTENGA siku ya Jumanne katika kila wiki kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa kero za ardhi katika jiji la Mbeya 

Amewataka watendaji wote katika halmashauri zote na taasisi zote za serikali mikoa was Mbeya kuwa karibu na wananchi na kushughulikia kwa haraka kero za wananchi badala YA kuwakwepa na amekemea kauli za njoo kesho zinazotolewa na watendaji wa serikali



0 comments:
Post a Comment