Posted by Williammalecela.com on Thursday, September 15, 2016
 |
Mjane wa mhubiri wa Kiislamu
aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana miaka minne iliyopita
amefikishwa mahakamani
Mombasa kuhusiana na shambulio lililotekelezwa
katika kituo cha polisi Mombasa Jumapili.
Bi Hania Said Saga Rogo alikamatwa Jumatano jioni na maafisa wa usalama.
Taarifa zinasema alikuwa na uhusiano na mmoja wa wanawake watatu waliouawa wakati wa shambulio hilo.
Bi
Saga ni mjane wa marehemu Aboud Rogo, ambaye alituhumiwa na vikosi vya
usalama vya Kenya na nchi Magharibi kwamba alihusika katika kusaidia
watu kujiunga na kundi la al-Shabab nchini Somalia. |
 |
Aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya kutoka Mombasa kwenda Malindi tarehe 27 Agosti, 2012.
Kuuawa
kwake kulisababisha ghasia zilizodumu siku kadha mjini Mombasa. Wakati
wa maandamano hayo, guruneti lilirushwa kwenye lori la polisi na
kusababisha vifo vya watu wawili. |
0 comments:
Post a Comment