M
SANII wa Bongo Fleva anayetamba kwa sasa na Wimbo wa Jike Shupa,
Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amesema kuwa kwa sasa amechoka kutegemea
skendo za kijinga kumng’arisha badala yake atajitahidi kuboresha kazi
zake akiamini hiyo ndiyo njia pekee ya mafanikio.
Nuh
aliyasema hayo alipokuwa akipiga stori na gazeti hili ambapo alisema
kama ni skendo amefanya sana lakini matokeo yake anaona maendeleo yake
kimuziki yanajongea kwa mwendo wa kobe suala ambalo ‘sometimez’
linamkatisha tamaa.
“Sasa
nataka nikomae tu kwenye kazi yangu ya muziki, kiki za kijinga hazina
faida, watu wanataka muziki mzuri tu na ndicho nitakachofanya ili
niwakune mashabiki wangu,” alisema Nuh.
0 comments:
Post a Comment