Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne
Maghembe, amesema kipaumbele chake kikubwa kitakuwa ni kupambana na
ujangili nchini
“Niwaambie majangili sasa wakafanye kazi nyingine ama wakae nyumbani,
kiama kinakuja huko, jambo la pili nitakaloshughulikia ni misitu,
kuitunza na kupambana na usafirishaji wa magogo na ukataji wa mkaa,”
alisema Profesa Maghembe.
Alisema kuwa atasimamia kwa uhakika maliasili za Watanzania kwa
sababu mambo ya maliasili ndiyo eneo alilobobea kwenye usomi wake.
“Tutajitahidi pia kutangaza utalii na kuongeza mapato ya sekta hii
kama tulivyofanya kwenye miaka ya 2006 hadi 2008, tuliongeza bei za
vitalu na ada kwa mnyama mmoja mmoja anayewindwa,” alisema Profesa
Maghembe.
0 comments:
Post a Comment