Mkuu wa huduma ya magereza katika
mji Buenos Aires Argentina amefutwa kazi baada ya wafungwa watatu
mashuhuri walioshikiliwa gerezani hapo kwa makosa ya mauaji kutoroka kutoka gereza lenye ulinzi mkali siku ya Jumapili....,
Wafungwa hao Victor Schillaci na kaka wawili Cristian na Martin Lanatta, walikuwa wanatumikia hukumu ya maisha gerezani kwa makosa ya utekaji nyara na mauaji ya wafanyabiashara watatu katika tukio lililohusishwa na mzozo wa madawa ya kulevya mnamo mwaka wa 2008.
Wafungwa hao walitoroka kutoka kwenye gereza lenye ulinzi mkali huku wakitumia bunduki bandia kutishia mmoja wa walinzi wa gereza hilo.
0 comments:
Post a Comment