Justin Bieber.
KAMA wewe ni mdau wa burudani, Jina la JUSTIN BIEBER
linaweza lisiwe geni masikioni mwako hasa kutokana na umaarufu mkubwa
alioupata kupitia kipaji chake cha uimbaji tangu akiwa kijana mdogo.
Hata hivyo, wakati staa huyo akizidi kujipatia mafanikio, mashabiki
wake wengi waliokuwa wakimchukulia kama mfano wa kuigwa wamembadilikia
kwa kumuona kama mtu asiyefaa kuigwa na jamii hasa watoto wadogo
kutokana na vituko anavyovifanya kila kukicha visivyoendana na maadili
ya nchi nyingi hasa za Kiafrika.
Kwa mujibu wa wasifu wake, Justin Bieber anatajwa kukulia katika
maadili ya Kikristo na familia ya kawaida kabla ya kuukwaa umaarufu wa
ghafla kupitia nyimbo zake ambapo staa huyo amebadilika kabisa huku kila
mara akiripotiwa kwenye vyombo vya habari kwa kufanya vituko vya kila
aina vinavyoonesha jinsi gani amekengeuka tofauti na malezi aliyokulia.
Wachambuzi mbalimbali wa masuala ya burudani wamekuwa wakimtolea
mfano Bieber kama mwathirika wa mambo matatu ambayo ni; umaarufu
uliopindukia na pesa nyingi tofauti na umri wake vitu ambavyo kwa pamoja
ni hatari kwa msanii kama yeye kwa kuwa ni rahisi kuingia katika tabia
hatarishi kama matumizi ya madawa ya kulevya na tabia nyingine za
ajabu.Vifuatavyo ni baadhi ya vituko vya staa huyo:
Adakwa akivuta bangi Januari 2, mwaka 2013 Bieber alidakwa kwa
shutuma za kuvuta bangi na kunywa vilevi ndani ya chumba cha hoteli
iliyomo ndani ya Ufukwe wa Newport, Marekani pamoja na rafiki yake
mkubwa Lil Twist, hata hivyo baadaye aliachiwa huru.
Baada ya tukio hilo Bieber aliachia Kibao cha To Be Better chenye maudhui ya kuwaomba msamaha mashabiki wake kwa kitendo hicho.
Ampiga paparazi Akiendeleza mnyororo wa vituko vyake Bieber amewahi
kuingia katika skendo iliyomchafua zaidi baada ya kumchapa kibao
paparazi huko London alipomfuata kwa lengo la kumpiga picha, hata hivyo
baada ya paparazi huyo kucharuka, Bieber aliingia ndani ya gari lake na
kutokomea huku akiporomosha matusi.
Ajisaidia haja ndogo kwenye ndoo ya kupigia deki hotelini Kati ya
vituko vya Bieber vilivyowahi kuwashangaza wengi ni kile cha kujisaidia
haja ndogo kwenye ndoo ya kupigia deki katika chumba cha kulala wageni
kwenye hoteli moja maarufu jijini New York, sambamba na kusambaza picha
akifanya tukio hilo huku akimtukana aliyewahi kuwa Rais wa Marekani,
Bill Clinton. Hata hivyo, taarifa baadaye zilidai dogo huyo alifanya
hayo akiwa amelewa.
Atangaza kuacha muziki Mwishoni mwa mwaka 2014, Bieber aliwaacha
midomo wazi wapenzi wake baada ya kutangaza kuacha rasmi muziki. Baada
ya kuposti taarifa hiyo kwenye mtandao wake wa Twitter mashabiki wake
walimjia juu kwa kumponda lakini baadaye alipofanya mahojiano na gazeti
la kila siku la New York alidai kuwa taarifa hizo alizitoa kama utani.
Anunua machangudoa Iliwahi kuripotiwa alipokuwa kwenye ‘tour’ nchini
Brazil,Bieber alichepuka kwa kumsaliti aliyekuwa mpenzi wake Selena
Gomez baada ya kwenda kutalii kwenye mji wa Rio de Janeiro
alikoibuka na machagudoa wawili ambao alirudi nao hadi hotelini.
0 comments:
Post a Comment