Na
Haruni Sanchawa MAPENZI kiboko! Juma Ally, mkazi wa Mongolandege Ilala
jijini Dar es Salaam, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kumwagiwa
maji ya moto na mpenzi wake, Swaumu Shemsanga, kisa kikidaiwa kupishana
kauli kwenye mazungumzo yao.
Juma
Ally akionyesha jeraha alilolipata baada ya kumwagiwa maji ya moto na
mpenzi wake. Chanzo makini kimelieleza gazeti hili kuwa tukio hilo
lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Juma kwenda kwa rafiki
yake huyo na katika mazungumzo hayo, kudaiwa kuwa mwanaume alimwambia
mpenziwe kuwa huo ndiyo umekuwa mwisho wa mapenzi yao.Inadaiwa kuwa baada ya kauli hiyo, mwanamke huyo alimmwagia maji ya moto mpenzi wake, ambayo wakati wa mabishano alikuwa akiyachemsha.
Polisi walifungua jalada lenye namba GMT/RB/1682/2015 KUJERUHI, ingawa taarifa kutoka hospitalini hapo hazioneshi aliungua kiasi gani.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka hospitalini hapo, Juma alisema yeye ana mke na watoto, lakini Swaumu alikuwa ni mpenzi wake wa nje na wakati akienda nyumbani kwake, mkewe alikuwa safarini Morogoro.
Taarifa za kipolisi zinasema, Swaumu alikamatwa saa chache baada ya tukio hilo na uchunguzi wa suala hilo unaendelea.
0 comments:
Post a Comment