,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, June 16, 2015


KUZALIWA MASKINI SI KOSA LAKO, LAKINI KUFA MASKINI NI KOSA LAKO MWENYEWE.

Je wewe umeajiriwa? Unalipwa kiasi gani kwa mwezi? Na je kiasi unacholipwa kinatosha mahitaji yako na kutengeneza future yako? Kama mshahara wako hautoshi unafanya lolote kuhakikisha unakuza kipato chako?


Hata kama umeajiriwa na unalipwa "mamilioni" kwa mwezi usibweteke.. tafuta fursa ya biashara fanya.. siku hizi hadi mawaziri wanafanya ujasiriamali.. gavana wa BOT ni mjasiriamali mzuri tu. Sasa wewe daktari wa "digrii" umeajiriwa Mwananyamala Hospital unalipwa tumilioni tumoja unajiona umeula.. unaona wewe ni msomi na biashara ni za waliofeli shule. Badili mtizamo otherwise utakufa maskini.
Na kuna wale "kauka nikuvae" wanalipwa laki 5 kwa mwezi na wamebweteka tu na kuridhika na hali za maisha yao.. Hivi unajua laki 5 kwa mwezi ni sawa na Tsh 1,850 kwa saa? yaani dola moja. Ina maana umesoma mpaka chuo kikuu halafu thamani ya lisaa lako moja ni dola moja tu!!!!?
Ndiyo maana watu wengi waliosoma sana huwa hawawezi kuwa matajiri kwa sababu wanauza muda wao kwa "bei chee" halafu siku zinazidi kuyoyoma haoni mafanikio. Huku tena ana mkopo wa gari nk. Makato na marejesho... Kwa nini usife masikini kwa style hiyo.?

Shida ni kwamba watu wanaabudu sana kuajiriwa na wako tayari watoe hata rushwa ya ngono (kwa wadada) ili tu eti wajiriwe. Ajira imekuwa kama Mungu kwa wengine. Wanafunzi vyuoni wanasubiri kwa hamu kumaliza shule ili wakaajiriwe reception kupokea simu na kukaribisha wageni.. Seriously??
Halafu unasema umasikini unasababishwa na sijui na Richmond, mara sijui Escrow.. Hivi unajitambua kweli.?? Halafu mnapost vikatuni vya ‪#‎Shemeji_Unatuachaje‬? Hujui mtumaini cha shemeji hufa fukara!.
Sikia... maisha bora ni maamuzi yako binafsi. Hapo ulipo kuna watu wanakuuzia vitu kila siku.. kuanzia dawa ya meno, sabuni, nguo za ndani, suti unazovaa ofisini hadi chakula unachokula.. wewe unaona sifa tu kila ukipita wanakuita "boss" kisa wanakuuzia kila kitu.. Umewahi kujiuliza wewe unawauzia nini.??
Au ndo na wewe ndo umeamua kuuza muda wako kwa bosi kwa kulipwa laki 5??. Halafu unashangaa baada ya miaka 10 tangu uanze kazi bado unaishi nyunba ya kupanga.. huwezi kusomesha watoto wako shule bora wala huwezi kusafiri ukapumzike na familia Marekani, S.Africa au hata hapo Ngorongoro tu..
Bado unakula ugali dagaa, wali njegere na bamia.. miaka 10 baada ya ajira.. siyo kwamba unapenda ila ni shida tu zinakulazimisha.

Sikiliza nikuambie.. Dont sell your time in cheap way. You will die poor. Utakaaje mwezi mzima unalipwa laki 5 na wewe ni graduate halafu umeridhika eti "maisha ndo haya".. Acha ujinga.. Kama umeamua kuuza muda wako basi let it be expensive. Ulipwe ghali.. na usiuze muda wote.. bakiza muda wa kukutosha kufanya ujasiriamali nje ya kazi.
Kuna "vijitu" vinalipwa laki mbili na nusu kwa mwezi halafu vinatumia vocha ya laki moja kuingia Facebook kumsifia Wema Sepetu ambaye hakujui hata jina. Sijui ‪#‎Team_Zari‬ mara ‪#‎Team_Wema‬.. yani ni ujinga ujinga tu.. Hivi Watoto wako watakula comment zako au? Au hiyo #Team_Wema na ‪#‎Zari‬ itakusaidia kulipia ada wanao??

Mbaya zaidi "wenye akili" tukiandika mambo haya vitatokea "vikaragosi" vya kupinga na kutukana.. Na vingine wala havitasoma huu ujumbe.. na vikisoma vitapuuza..
Wewe unayesoma hapa leo Chukua hatua ndugu! Kumbuka maisha ni ya kwako na ni WEWE tu ndiye utakayeyabadili! Kila siku kunapokucha jiulize umefanya nini kupiga hatua ya maisha yako kutoka pale ulipokua jana. Jiulize maswali ya msingi na uchukue hatua.!

Change today. Usipobadilika utakufa maskini! Chukua hatua mpya ili upate matokeo mapya!
 
Acha wanaolalamika waendelee kulalamika. Bill Gates anasema: "KAMA ULIZALIWA MASKINI SIYO KOSA LAKO, LAKINI KAMA UKIFA MASKINI HILO NI KOSA LAKO"
Hakikisha unarudia kusoma ujumbe huu mara nyingi uwezavyo na hakikisha unashare na wengine.!

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi