,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, June 16, 2015


TANZANIA NCHI YA KUSADIKIKA.?

By Malisa GJ,

Tanzania bhana.. hii nchi ina vituko vyake very unique. Tunaishi kama nchi ya kusadikika vile... Eti wakubwa flani walikaa wakaona njia ya kupunguza foleni Dar ni kununua boti ya kwenda Bagamoyo. Itasaidia kupunguza msongamano New Bagamoyo Road kwa waendao Mbezi Beach, Tegeta, Bokko na pia wasafiri wa Bagamoyo watafika haraka.


Boti ikanunuliwa. Nimeiobserve pale Ferry inatumia masaa mawili na nusu kufika Bagamoyo kutokea Dar and itz vice versa; while kwa bus ni one hour na kwa self drive ni less than an hour. Last week nimetumia nusu saa kudrive Dar to Bagamoyo na nusu saa kurudi. Tafsiri yake ni kwamba ukiwa na gari binafsi unaweza kwenda Bagamoyo na kurudi mara 5 ndio Boti ifike. Ina speed ndogo kuliko trekta.

Sasa baada ya serikali kuona "gia" ya mwendokasi imefeli, wamekuja na mpya nyingine. Waziri wa Uchukuzi akijibu hoja bungeni amesema lengo la kununua boti sio usafiri wa haraka tu bali pia ni "adventure na starehe" kwa wasafiri.
Hivi kweli Bagamoyo Dar ni adventure? Kama mtu anataka adventure si apande pantoni ya Mv.Magogoni ashinde huko siku nzima bila kushuka.. Hata hivyo je hiyo boti ina mazingira ya kuenjoy na kufanya adventures? Boti watu wanapanda na kuku, samaki, pweza, ngisi, nazi, na mananasi ndio adventure?

Boti inazidiwa mbali mno na Kilimanjaro IV ya Bakhresa. Bora hata watu wapande Kilimanjaro IV wanaweza kupata adventure sio hiyo boti ya serikali ambayo inaweza kuzima anytime katikati ya maji. Boti ya Bakhresa inatumia dakika 90 kutoka Dar hadi Zanzibar, boti ya serikali inatumia masaa mawili na nusu kufika Bagamoyo afu tunaambiwa ni adventure. Hivi hii ikienda Zanzibar si itatumia wiki nzima?

Sasa naanza kumuelewa Mkosamali aliposema ukitaka matatizo nchi hii tumia vitu vya serikali. Yani ni aibu.. Mtanzania hana ajira, hana hela ya kula, hana ada ya kulipia wanae shule, hana kodi ya nyunba, halafu eti unamletea boti ya kufanya adventure? Hivi serikali ya CCM huwa inafikiria kabla ya kufanya maamuzi??
Halafu kichekesho nasikia imenunuliwa "ghali" zaidi kuliko Kilimanjaro IV ya Bakhresa.! Eeh Mungu tunusuru na janga la CCM.

Malisa GJ.!

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi