NABII wa Kanisa la The Revelation Church lililopo Buza-Kipera jijini Dar, Yaspi Bendera amesema anao uwezo wa kumponya kwa maombi msanii wa Bongo Muvi anayesumbuliwa na tatizo la kutopata mimba, Wema Sepetu.
Msanii wa Bongo Muvi Wema Sepetu. Akizungumza na mwandishi wetu kupitia msemaji wake, Nabii Yaspi alisema mwanamke yeyote aliyevunja ungo, amepewa na Mungu uwezo wa kuzaa isipokuwa shetani huingilia kati na kumnyima furaha mwanamke husika.
“Endapo ndani ya muda huo atashindwa kupata ujauzito, nipo tayari kuacha utumishi na kurejea zangu kijijini kuendelea na maisha mengine, maana kazi hii ni ya kiroho ambayo tunapewa maono na Mwenyezi Mungu,” alisema Nabii huyo.
0 comments:
Post a Comment