Baadhi ya majeruhi ambao walisafirishwa kwa njia ya ndege kutoka Garissa wamewasili ili kupata matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta mjini Nairobi Kenya.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametuma risala za rambi rambi kwa familia za wale waliouawa katika shambulizi la chuo kikuu cha Garissa kazkazini mashariki mwa Kenya.Kiongozi huyo vilevile amewahakikishia wakenya kwamba serikali yake imechukua hatua za kuwapeleka maafisa wa usalama katika eneo hilo.Amewataka wakenya kuwa watulivu wakatu huu ambapo maafisa wa usalama wanakabiliana na wapiganaji hao.
Waziri wa maswala ya ndani nchini Kenya Joseph Nkaiserry amethibitisha kuwa watu 15 wameuawa huku wengine 53 wakijeruhiwa kufuatia shambulizi la alfajiri katika chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya.miongoni mwa waliokfariki ni walinzi wawili wa mlango wa chuo hicho.Akizungumza kutoka Garissa Nkaiserry amesema kuwa oparesheni ya kuwasaka wahalifu hao itaendelea hadi mateka wote waokolewe.
Wanafunzi wa chuo cha Garissa
Wanafunzi walio fanikiwa kutoroka
Askar wa kenya wakifa wanasogea maeneo ya chuo
Kundi lililoshambulia chuo cha Garissa wakiwa eneo la nje







0 comments:
Post a Comment