,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, April 15, 2015



Serikali ya Kenya imeahidi kuwasamehe wakenya ambao wamepokea mafunzo ya kigaidi endapo watajitokeza katika kipindi cha siku 10 zijazo.


Waziri wa usalama wa ndani jenerali mstaafu Joseph Nkaissery pia amewaonya wazazi wa vijana kama hao kwamba watachukuliwa hatua kali endapo hawataijulisha serikali kuhusu kujiunga kwa wanao na kundi la Al Shabaab.

Serikali imewapa wale wote waliopokea mafunzo kutoka kwa Al Shabaab siku kumi kupiga ripoti kwa afisi za wasimamizi wa miji ya Garissa, Mombasa ama Nairobi.
Kenya imechapisha nambari za simu ambazo wakeAl Shabaab ilikiri kutekeleza shambuliz ambalo wakristo 147 waliuawa katika chuo kikuu cha Garissa
Wazazi ambao wanao wametoweka, au wanaojua kuwa wamejiunga na Al Shabaab ama kuuwawa nchini Somalia wametakiwa kutoa ripoti hizo kwa serikali la sivyo wafunguliwe mashtaka kama washiriki wa magaidi.

Hofu imeibuka nchini Kenya baada ya ripoti kwamba mmoja wa wanamgambo walioshambulia chuo kikuu cha Garissa na kuchangia kuwaua watu 147 alikuwa Mkenya aliyesomea taaluma ya sheria jijini Nairobi. Babake, ambaye ni chifu, alipiga ripoti kwa serikali alipotoweka mwanawe miaka miwili iliyopita.

BBC

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi