MAMA
Fanueliii! Mwanamke Elgiva Winyaeli Munisi ‘Manka’, mkazi wa
Kijitonyama, Dar, amejikuta katika wakati mgumu baada ya mumewe, Alpha
kudaiwa kuzinasa picha za utupu akiwa na mchepuko uliofahamika kwa jina
la Crama Lucas ambaye ni msanii wa Bongo Muvi, Ijumaa Wikienda lina
filamu kamili.
Chanzo makini kimeliambia gazeti hili kwamba, awali,
mwanaume huyo alizibamba picha chafu za mwanaume peke yake zikiwa kwenye
laptop ya mkewe ambapo alipomuuliza alijitetea si zake ni za rafiki
yake alimtumia yeye kupitia Mtandao wa WhatsApp.
Elgiva Winyaeli Munisi ‘Manka’ na mchepuko wake Crama Lucas ambaye ni msanii wa Bongo Muvi, wakipozi kimahaba.
MUME AJIONGEZA
Iliendelea
kudaiwa kuwa, mume alimuuliza rafiki aliyetajwa ambapo awali alikataa
kumtumia picha hizo Manka, lakini baadaye alikiri jambo ambalo mume
alijiongeza akiamini lilipangwa.
MACHALE YAMCHEZA
Ilidaiwa kuwa, mume alimkalisha mkewe na kumwambia alichofanya ni kosa kubwa katika ndoa, mambo yakaisha.
Chanzo
kilitiririka: “Lakini mume akawa bado machale kama yanamcheza kwani
aliingiwa na wasiwasi mkubwa kuamini kuwa, mkewe anaweza kuhifadhi picha
chafu za mwanaume kwenye laptop.
“Siku moja, mumewe alikwenda kwenye
stationery (duka la vifaa vya kuandikia) inayomilikiwa ya dada yake
Manka (jina tunalo) maeneo ya Sinza-Mori (Dar).
“Alipofika aliwauliza
wafanyakazi kwamba mkewe akienda pale hukaa kwenye kompyuta gani!
Wakamwonesha, akakaa, akasachi jina la mkewe likatokea folda lenye picha
kibao za mkewe huyo akiwa na Crama tena kwenye mapozi ya kimahaba.
MUME APAGAWA
“Palepale
mume alipagawa, kidogo presha imshike. Alimpigia simu mkewe akamuita
aje pale alipo lakini mke alisema ana kazi nyingi nyumbani hawezi
kutoka. Mume alitoka hadi nyumbani kwake na kumuuliza mke wake kuhusu
picha hizo, mke akadai mwanaume huyo ni mteja wake wa mashuka! Mh!
“Hasira
zilimpanda mwanaume, mteja gani wa mashuka hadi kupiga picha? Alimpiga
mkewe hadi kumpasua sehemu ya paji la uso na kumchomea nguo moto. Mke
akakimbilia Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar kushitaki
lakini baadaye alifuta kesi.”
MUME ASAKWA
Baada
ya madai hayo, Ijumaa Wikienda lilimsaka Alpha, alipopatikana alikiri
kuwepo kwa mgogoro kati yake na mkewe chanzo kikiwa ni hizo picha chafu
alizopiga mkewe na zile alizopiga akiwa na mwanaume anayedaiwa kuwa
ndiye mchepuko wake.
“Awali, nilizifuma picha za utupu za mwanaume
nikaamua kumpeleka mke wangu kwao akapumzike lakini wazazi wake
walimuonya, akarudi tukawa tunaendelea na maisha, sasa sijui amekumbwa
na nini mpaka leo hii akatoka nje ya ndoa wakati mimi nipo na
ukizingatia ni mtu ambaye nimetoka naye mbali.
“Mpaka nazikuta hizi
picha sikuamini kabisa kama mke wangu anaweza kunifanyia hivi. Sijui
walipigaje kwanza, lakini niliumia sana nikaamua kumpiga mpaka
akachananika usoni na nilimchomea nguo zake zote kwa sababu nilikuwa
nina hasira.”
MUME BADO
“Tangu siku hiyo mke wangu aliondoka
nyumbani, mpaka sasa hivi anaishi kwa dada yake lakini kila nikimuomba
arudi nyumbani anakataa na kudai kuwa anaogopa nitampiga, ila
nilishaongea na yule mwanaume na nikamtaka tuonane akaniambia hawezi
kuonana na mimi.
“Pamoja na yote, bado ninampenda mke wangu kwani sitarajii kufunga ndoa na mwanamke mwingine,” alisema Alpha.
Kuhusu uhai wa nyumba yao, Alpha alisema alifunga ndoa na Manka mwaka 2009 katika Kanisa la Anglikana Chimuli, Dodoma.
CRAMA ASAKWA
Kwa upande wake, Crama alipotafufwa kwa simu na gazeti hili kuhusu madai hayo, alisema:
“Mimi
na Manka tunafahamiana kwa muda mrefu tena ni rafiki yangu kwa sababu
tulifahamiana kupitia Mtandao wa Kijamii wa Instagram na alikuwa
akinikopesha mashuka.
“Alikuwa anakuja sana nyumbani kwangu kudai
madeni yake lakini yeye mwenyewe ndiyo alikuwa akinishinikiza tupige
picha tena kwa kutumia simu yake.
“Sikujua kama ni mke wa mtu wala
yeye mwenyewe hakuwahi kuniambia kama ameolewa na wala hakuwa na pete ya
ndoa, ila nilishawahi kumwambia kuwa picha tunazopiga zisije zikazua
balaa baadaye, hakuonesha mshtuko.
“Niliwahi kupigiwa simu na mume
wake akidai kuwa nilikuwa nikimuibia mke wake, kumbe si kweli kwa sababu
Manka mwenyewe anamfahamu mchumba wangu.”
HUYU HAPA MANKA
Manka
alipotafutwa juzi kujibu tuhuma hizo kupitia simu yake ya mkononi alidai
kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo kwa muda huo mpaka atakapojipanga:
“Siwezi kuliongelea hilo sasa hivi mpaka pale nitakapojipanga na kujua hizo picha zimefikaje hapo ofisini kwenu.”
0 comments:
Post a Comment