RAPPA,
komedian na mwigizaji wa Marekani, Nicholas Scott "Nick" Cannon ameamua
kumfutilia mbali mkewe wa zamani Mariah Carey kwa tattoo nyingine zaidi
mgongoni mwake.
Awali
Nick Cannon (34) aliamua kufuta tattoo ya jina la mkewe Mariah Carey
aliyeachana naye mwaka jana kwa tattoo ya mchoro wa Yesu akiwa
msalabani.…

msalabani.
Kuona
kuwa hiyo haitosha, staa huyo ameamua kuongeza tattoo zaidi ili
kumwondoa kabisa mkewe huyo akilini ambapo ameongeza michoro mingine
mgongoni ikiambatana na maneno haya kwa chini "Baba, wasamehe watu hawa
maana hawajui walifanyalo" maneno ambayo yatakuwa yanahusiana na ndoa
yake na Mariah.
Cannon na Mariah walifunga ndoa mwaka 2008 na kudumu kwa miaka sita kabla ya kuachana mwaka jana.
Katika mahusiano yao walifanikiwa kupata watoto wawili mapacha Monroe na Moroccan.
0 comments:
Post a Comment