Posted by Williammalecela.com on Tuesday, March 17, 2015
 |
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe.Anna Makinda amesema anamtambua Mbunge wa Kigoma
Kaskazini Zitto Zubeir Kabwe kuwa ni mbunge halali kutokana na ofisi
yake kutokuwa na taarifa rasmi kutoka tume ya Taifa ya Uchaguzi
kuhusiana na ubunge wake kutenguliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya bunge Spika
Makinda amesema kuna taratibu zilitakiwa kufuatwa ambapo mpaka sasa
taratibu hizo hazijakamilika na kumfanya kumtambua kuwa ni mbunge halali
wa jimbo hilo la Kigoma Kaskazini
|
0 comments:
Post a Comment