Takriban miezi mitatu tangu sakata la uchotwaji wa fedha zaidi ya
Sh. bilioni 200 katika akaunti ya Tegeta Escrow kutikisa nchi huku
mawaziri wawili na mwanasheria mkuu wa serikali wakiondoka madarakani,
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe,
amefichua kuwa wajumbe wote wa kamati hiyo wataadhibiwa vibaya kwenye
majimbo yao kama njia ya kulipiza kisasi kutokana na kuwaumbua wote
walionufaika na fedha hizo.
Katika
mahojiano na kituo cha ITV kwenye kipindi cha Dakika 45, kilichorushwa
jana usiku, Zitto amesema kuwa wakati PAC wakiendelea kuchambua ripoti
ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) juu ya Escrow,
mjumbe mmoja wa kamati hiyo aliitwa na ‘wakubwa’na kuelezwa kwamba
akifika bungeni awageuke wenzake na aseme kuwa mgogoro wa ripoti ya
Escrow iliandikwa kwa shinikizo la mfanyabiashara mmoja.
Aliongeza
kuwa mjumbe huyo alipokataa aliambiwa: “ Umekataa kutekeleza hili? Sasa
tumetenga Sh. milioni 500 kwa kila jimbo kwa kila mjumbe wa PAC ili
kuhakikisha hawarudi bungeni.”
Nini maoni yako kuhusu hili?
CHANZO: East Africa Radio

0 comments:
Post a Comment