MDADA
mwenye figa namba nane kunako gemu ya Bongo Fleva, Meninah, jana
ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa (birthday) kwa aina yake katika
viwanja vya Hekima Garden vilivyopo Mikocheni B jijini Dar.
Katika
birthday hiyo wasanii kadhaa wakiwemou Kadjanito, Shilole, Nuh
Mziwanda, JI na Queen Darleen walikuwepo kumpa sapoti ya nguvu msanii
mwenzao huyo katika sherehe hiyo iliyopambwa na mbwembwe kibao.
Miongoni mwake ni keki zilizokuwa na maumbo ya piano na gitaa na kisha
kufuatia shoo kali kutoka kwa mwanadada huyo.
0 comments:
Post a Comment