Kanye West
anafahamika kwa kuwatoa wasanii wengi wakubwa nchini Marekani. Bila yeye
leo hii hakuna mtu angekuwa anawajua Big Sean na John Legend.Na
sasa kupitia ngoma yake mpya ‘All Day’, (ambayo hakuna shaka itakuwemo
kwenye album yake mpya), Yeezy anamweka kwenye ramani ya muziki duniani,
rapper Mtanzania aishiye Minnesota, Marekani, Allan Kingdom.Hakuna mkazi wa Minnesota asiyemjua rapper huyu na infact ni supaster tayari pande hizo japo tunasikitika kuwa tumemfahamu sasa kupitia Kanye West aliyemshirikisha kwenye ngoma yake ambayo tayari
Kinachofurahisha zaidi ni kuwa Kanye amempandisha rapper huyo jana (Jumatano) kwenye Brit Awards (zenye level sawa na tuzo za Grammy za Marekani) zilizofanyika jijini London kutumbuiza ngoma hiyo. Tuzo hizo zimehudhuriwa na mastaa wote wakubwa unaowajua wakiwemo Kim Kardashian, Taylor Swift, Lionel Richie, Sam Smith kutaja wachache tu.
Kwa mujibu wa Star Tribune, Kanye atakuwa amemfahamu Allan kupitia mkurugenzi wake wa ubunifu, Virgil Abloh ambaye ni sehemu ya watu walio kwenye kambi ya Allan. Hakitakuwa kitu cha ajabu kama akishawishika pia kumuongeza kwenye list ya wasanii wa label yake, GOOD Music.

credit bongo5

Lol!
ReplyDelete