Wadau wanaopaswa kujisajili na kuhakikisha wanakuwa na vibali vya kuendesha shughuli za Sanaa ni pamoja na wasanii binafsi, vikundi vya wasanii,Bendi za muziki, wakuzaji Sanaa maarufu kama Mapromota/m
ameneja, studio za kurekodi muziki na wamiliki wa kumbi zinazotumika kwa ajili ya maonesho ya shughuli za Sanaa zikiwemo disko, harusi na sherehe mbalimbali zenye kupambwa na sanaa ama burudani.
Zoezi hili la usajili na utoaji vibali ni sehemu ya mkakati wa Serikali kuirasimisha sekta ya Sanaa kwa kuwatambua wadau wote wanaojishughulisha na kazi za Sanaa ili waweze kufanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria, kanuni, maadili na taratibu zilizowekwa na kuepuka uholela jambo ambalo ni moja ya chanzo cha wizi wa kazi za wasanii, mmomomyoko wa maadili udanganyifu katika mikataba ya kazi za Sanaa na changamoto nyingine zinazotokana na shughuli za Sanaa na kupelekea ugumu kwa Serikali wakati wa kutatua changamoto hizo
Kaimu Katibu Mtendaji amefafanua kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Bunge namba 23 ya mwaka 1984 ni kosa Kisheria kwa wadau wa Sanaa kuendesha shughuli zao bila kusajiliwa na kupata kibali toka BASATA.
Aidha, anasisitiza kwamba ili kuepuka usumbufu ni vema wadau wote ambao hawajasajiliwa na wale ambao hawajahuisha vibali vyao kuhakikisha wanafanya hivyo mapema iwezekanavyo ili kuepuka usumbufu usio wa lazima.
Sanaa Ni Kazi, Tuikuze Na Kuithamini
Godfrey Mngereza
Katibu Mtendaji (K)
0 comments:
Post a Comment