KUTOKANA na vifo vya mara kwa mara
vya wasanii, staa wa filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ameibuka na
kusema ni wakati wa wasanii kumrudia Mungu.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi
karibuni, Dude alisema kwa kipindi kifupi vimetokea vifo vingi vya
wasanii tena wenye umri mdogo, hivyo anawataka wasanii wabadili mfumo
wao wa maisha kwa kuachana na mambo maovu, anasa za dunia kwani hawajui
siku wala saa ya kufariki dunia.
“Wasanii tunazidi kufa, juzi
tumemzika Ngwea, leo tena Kashi wasanii tunatakiwa kufanya ibada, wenye
sauti za kuimba wamwimbie Mungu kwani waliotangulia hawakujua kama
watakufa, binafsi nimeanza kusali tangu nilipofiwa na mama yangu,”
alisema Dude.

0 comments:
Post a Comment