Uchaguzi wa Madiwani wa Kata nne za Jiji la Arusha uliokua ufanyike
leo umeairishwa hadi tarehe 30/06/2013 mwaka huu,uchaguzi huo
umeahirishwa kufuatia shambulio la kigaidi lililotokea jana katika
Mkutano wa kufunga kampeni ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema).
Akizungumza na Habarimpya.com jijini Arusha
Mkurugenzi wa Jiji hilo Sipora Liana amesema uchaguzi huo umeairishwa
kutokana na sababu za Kiusalama,na kwamba utafanyika katika tarehe hiyo
endapo hali itatulia.
"Tumelazimika kuahirisha uchaguzi huo kwa sababu za kiusalama,
hatuwezi kuendelea na uchaguzi katika hali kama hii, hali si shwari
katika Jiji la Arusha na hata tarehe hiyo iliyopangwa pia inaweza
ikaahirishwa endapo hali haitakuwa shwari"alisema Liana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema
katika tukio hilo watu wawili mwanamke na mwanamume wamepoteza maisha,
huku akidai kwamba bado wanafuatlia idadi ya majeruhi waliotawanywa
katika Hospitali mbalimbali mkoani humo.
Hilo ni tukio la pili la bomu kulipuka katika mkusanyiko
wa watu wengi mkoani humo, Mei 5 mwaka huu bomu lililipuka katika Kanisa
Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit mjini Arusha
na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.

0 comments:
Post a Comment