MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka
kuwa, suala la wasanii wa muziki kurogana linamuumiza kichwa kiasi cha
kufikiria kuachana na kazi hiyo.
Shilole alisema hivi sasa ‘kesi’
za wasanii kurogana zimeshika kasi kuliko siku za nyuma na anashindwa
kuelewa ni kwa nini watu wanamuasi Mungu kwa kuendekeza ushirikina.
“Kwa staili hii wasanii tutazidi kupukutika, kuna wakati huwa nafikiria hata kuachana na muziki maana tunarogana na namuomba Mungu usiku na mchana hata kabla ya kupanda stejini kwani hali ni tete,” alisema Shilole.

0 comments:
Post a Comment