,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, May 31, 2013

Taarifa Muhimu Kwa Umma Kutoka Benki Kuu ya Tanzania


 Benki Kuu inapenda kuutahadharisha umma kuwa katika siku za karibuni kumekuwepo na mtandao wa matapeli unaotumia TOVUTI ifuatayo www.jakayafoundation.wapka.mobi/index.html . Mtandao huo unajidai kuwa ni Taasisi ya Fedha ijulikanayo kwa jina la Jakaya foundation ambayoinamilikiwa na Benki Kuu chini ya utawala wa bodi kuu ya mikopo inayotolewa na serikali kupitia sekretariat ya Utumishi wa umma ofisi ya Rais.
 
Matapeli hao wanaeleza kwamba Taasisi hiyo inatoa mikopo ndani ya masaa 24 kwa Mtanzania yeyotemwenye umri kuanzia miaka 18 endapo atajiunga kwa kulip a ada ya shilingi 37,000/=.BENKI KUU INAUARIFU UMMA KUWA HAIITAMBUI NA WALA HAIHUSIANI KWA NAMNA YOYOTE ILE NA TAASISI INAYOELEZWA KWENYE TOVUTI HIYO.
 
Kwa taarifa hii, Benki Kuu inatoa tahadhari kwa Wananchi kutojihusisha na Taasisi hiyo ya kitapeli kwa ajili ya kupata huduma za mikopo kama ambavyo inadai.
 
IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO NA ITIFAKI BENKI KUU YA TANZANIA DAR ES SALAAM. 29/5/2013

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi