DIAMOND AOMBA MSAMAHA KWA JOKETE
MKALI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameibuka na kuelezea
kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake zilipendwa, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
ambaye ni mwigizaji na modo moto wa kuotea mbali Tanzania.
![]() |
| Diamond Platnumz akiwa na Kidoti wakati wa mapenzi yao |
Akizungumza
kwa uhakika kabisa, Diamond alisema inampasa amuombe radhi Jokate kwa
sababu katika uhusiano wao, Jokate hakuwahi kumkosea ila yeye ndiye
tatizo na chanzo cha kuachana kwao.
Diamond alisema hayo kwenye mahojiano na Mtangazaji Zamaradi Mketema katika Runinga ya Clouds kwenye Kipindi cha Take One, kilichorushwa juzi Jumanne usiku kituoni hapo.
Diamond alisema hayo kwenye mahojiano na Mtangazaji Zamaradi Mketema katika Runinga ya Clouds kwenye Kipindi cha Take One, kilichorushwa juzi Jumanne usiku kituoni hapo.
DIAMOND ANAFAFANUA
“Inanipasa nimuombe radhi Jokate. Ni kweli nilimtenda vibaya wakati wa mapenzi yetu. Hakukosea sana maana hakuwahi kufanya jambo lolote kinyume. Sijui niseme nini lakini nataka kueleza wazi kuwa mimi ndiyo sababu ya kuachana kwetu na ilitokea tu.

| Mzee mzima akijiachia na baby wake huyo wa zamani |
“Naamini
hilo jambo lilimuuma sana, maana nakumbuka wakati ule, baada ya mimi
kurudi kwa Wema (Sepetu), watu walimwandama sana kwa maneno na
alionekana msaliti lakini ukweli ni kwamba nilimpenda sana lakini ndiyo
hivyo, siwezi kufafanua zaidi.
“Kutoka
moyoni mwangu, namuomba msamaha Jokate, kama hatanisamehe nitaendelea
kumuomba mpaka naingia kaburini. Sina raha kabisa kutokana na jambo
hilo. Lazima niwe mkweli.”
JACQUELINE WOLPER
Diamond
alikwenda mbali zaidi na kuwazungumzia baadhi ya wasichana aliowahi
kutoka nao kimapenzi akiwemo mwigizaji Jacqueline Wolper ambaye alisema
ni mwanamke aliyempenda sana, ndiyo maana alimtungia wimbo wa Mawazo.
PENNY SASA
Kwa
upande wa mpenzi aliye naye sasa, Mtangazaji wa Runinga ya DTV, Penieli
Mungilwa ‘Penny’ alisema ni mwanamke mtulivu na sahihi kwake kwa sababu
anatambua majukumu yake kwake, pia anamheshimu.
“Huyu
kwa kweli ana karibu sifa zote alizonazo Wema ila uzuri wa Penny
ananiheshimu sana. Hafanyi mambo yake hadharani. Unajua wakati nikiwa na
Wema hata kama akifanya mambo yake siku mbili au tatu baadaye nayaona
kwenye magazeti, tofauti na Penny ambaye kwangu mimi naona ananiheshimu,
hata kama anafanya mambo yake ni kwa siri.”

Huyu mtoto inaelekea alienda jando la hospitali.
ReplyDeleteKabisa hata akili
ReplyDelete