Baada
ya kumalizika kwa uchunguzi, uliokuwa ukifanyika katika hospitali ya
Hillbrow, mwili wa marehemu Albert Mangwea(Pichani) unatarajiwa kuwasili
Jumamosi kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika ya kusini, ukitokea
nchini Afrika ya kusini.
Mwili utapelekwa moja kwa moja katika hospitali ya muhimbili kuhifadhiwa, uletwaji wa mwili huo, ni kwa hisani ya Clouds Media Group. Ndio waliogharimia safari ya mwili wa marehemu.
Jumapili asubuhi, kuanzia saa mbili, mwili wa Albert Mangwea utakuwa unaagwa na hapa kampuni itakayoshughulikia zoezi hili ni Entertainment Masters na baada ya mwili kuagwa, safari ya kumsindikiza Albert Mangwea kuelekea kwenye maziko itanza, na hii itakuwa ni kuelekea Morogoro.
Mwili wa Mangwea utazikwa Jumatatu katika eneo la Kihonda, mkoani Morogoro.
Michango zaidi ya wadau inahitajika ambapo kwa tigopesa namba ni 0717 553 905
M pesa namba ni 0754 967 738

0 comments:
Post a Comment