Msimu wa 8 wa Big Brother Africa ‘The Chase’ unazidi
kushika kasi, sio tu kwa washiriki lakini hata kufichua nyeti za chini
ya kapeti ambazo kama si Big Brother leo hii huenda nisingekuwa naandika
habari hii.
Mume wa mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa nchini Uganda Zari
aitwaye Ivan Ssemwanga, mara baada ya show ya ufunguzi wa shindano la
Big Brother Jumapili (May 26) kuanza, alisema hataangalia Big Brother
baada ya kugundua kuwa mpenzi wa zamani wa mkewe Zari , staa wa
basketball aitwaye Isaac Lugudde LK4 ambaye ni mwakilishi wa Uganda yuko
mjengoni, hivyo ni kama tusi kwake.
Wakati akitazama ufunguzi huo kabla washiriki hawajafahamika, Ivan
alimuona mshiriki wa kwanza kupanda kwenye stage, bibie Pokello wa
Zimbabwe, ambaye alimchagua mpinzani wa Ivan aitwaye Isaac kama mwanaume
wa kuingia naye. Baada ya kitendo hicho Ivan aliamua kuswitch kwenye
movie na kutweet “Chillin in ma cinema room watching Temptations by
Tyler Perry” akiashiria haangalii tena BBA.
Uhusiano wa Zari na Isaac ulikuja miezi kadhaa iliyopita baada ya Zari na mumewe kuachana kwa muda na baadae walikuja kurudiana.
Siku moja baada ya reality show hiyo inayoendelea huko Afrika Kusini
kuanza rasmi, msichana mrembo na tajiri wa nchini Uganda ‘boss lady’
Zari Hussein alionyesha jeuri ya pesa kwa kusema hawezi kushindania
$300,000 za Big Brother ambazo hazifikii hata thamani ya moja ya magari
anayotumia ambayo ni $ 389,500!! Hey peeps! Huyu manzi anamiliki
Lamborghini among others.
0 comments:
Post a Comment