MWANAMUZIKI
Nasibu Abdul ‘Diamond’ hivi karibuni aliwachefua waumini wenzake wa
dini ya Kiislam baada ya kutinga kwenye Maulidi akiwa amevaa hereni na
cheni.
Tukio hilo lilijiri maeneo ya Tandale, Dar ambapo mama yake aliyemtambulisha kwa jina la Aunt Shani aliandaa maulidi kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu.
Akiwa mmoja wa waalikwa, Diamond alinaswa akiomba dua sambamba na rafiki
yake aitwaye Remeo Jones ‘RJ’ huku akiwa amevaa kanzu safi na
balaghashia lakini akaharibu kwa kuvaa hereni na cheni.
Kitendo hicho kiliwachefua Waislam ambapo baadhi walifikia hatua ya
kumchana laivu kuwa, alichokifanya kilikuwa kinyume na Uislam.
0 comments:
Post a Comment