LICHA ya ushindi wa Rais Barack Obama, nyuma ya pazia kuna taarifa kuwa, mzee mmoja ambaye ni mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la John Dimo (105) alimfanyia mambo ya kishirikina ili kumhakikishia ushindi.
“Baada ya kufanya ushirikina wake, alichukua majumba mawili ya konokono, moja akalipa jina la Romney na lingine jina la Obama kisha akatoka nje na kuyatupa mbali.
“Baada ya zoezi hilo, akayafuata na kukuta lile alilolipa jina la Obama liko mbele ya lile la Romney, akabaini kuwa ushirikina wake umefanya kazi na ndipo alipowatangazia watu kuwa, Obama atashinda bila kipingamizi,” alieleza jirani wa mzee huyo.
Hata hivyo, baada ya matokeo kutangazwa Jumatano iliyopita, mzee huyo alijipatia umaarufu mkubwa na watu waliomfagilia licha ya wengine kueleza kuwa, ushindi wa Obama umetokana na uchapakazi wake pamoja na kupendwa na watu na si mambo ya ushirikina.
0 comments:
Post a Comment