Simba, TFF walaani Kaseja kudhalilishwa
Imetumwa
Jumanne,Novemba6
2012
saa
23:56 PM
Kwa ufupi
"Uongozi umesikitishwa sana na kitendo cha mashabiki kuvamia basi la wachezaji Kibaha juzi na kutaka kumshusha Kaseja wampige na kumtukana matusi ya nguoni ikiwamo kumuita mchawi na ukoo wake siyo kitu kizuri,"alisema Kamwaga.
Vicky Kimaro
UONGOZI wa Simba, sambamba na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wamelaani kitendo cha mashabiki wa Simba kumtukana na kumdhalilisha kipa Juma Kaseja.
Akizungumza makao makuu ya klabu hiyo jana, ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema uongozi wa klabu hiyo unasikitishwa na mwenendo wa timu hiyo na tayari wamelitaka benchi la ufundi kuandaa ripoti juu ya hali hiyo.

Alisema,"Kaseja ameitumikia Simba kwa zaidi ya miaka 10 na amekuwa nahodha, kumfanyia fujo siyo ushabiki, Kaseja naye ni binadamu ukifika wakati wake ataondoka kama walivyoondoka akina Idd Pazi na Mohamed Mwameja ambao nao walikuwa ni makipa bora kabisa," alisisitiza Kamwaga.
"Tumecheza mechi 12 tukaongoza ligi, zikafululiza sare na baadaye kufungwa na Mtibwa Sugar, uongozi hilo uliliona na ndiyo maana wakalitaka benchi la ufundi kuandaa ripoti ili tuweze kufanya marekebisho, tujipange kwa mzunguko wa pili,"alisema Kamwaga.
Kamwaga alisema,"kushinikiza viongozi wajiuzulu siyo dawa na wala hakuna kiongozi yeyote ambaye amejiuzulu au atajiuzulu kwa sababu ya matokeo ya kufungwa mechi moja tu, tulikuwa pamoja wakati timu ikifanya vizuri na pia hatutaachana timu inapofanya vibaya."
Alisema,"uongozi huu upo madarakani mwaka wa tatu sasa, mwaka wa kwanza tulipoteza ubingwa, mwaka wa pili tukachukua ubingwa, na mwaka huu tunautetea, tuna mechi 13 za mzunguko wa pili, uongozi huu huu ndiyo umevunja rekodi kwa kuifanya Simba ionekane bora Afrika Mashariki baada ya kuingia kwenye 16 bora ya mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF)."
Kamwaga alisema,"mashabiki wa Simba wakumbuke Juventus ilimaliza ligi msimu uliopita na kuweka rekodi ya kucheza mechi 49 bila kupoteza, lakini juzi wakati Simba ikifungwa na wao walifungwa na Inter Milan 3-1, kwa hiyo kufungwa kwetu isiwe chanzo cha migogoro isiyokuwa na msingi."
Naye Katibu mkuu wa TFF, Angetile Osiah amelaani fujo hizo za mashabiki wa Simba na kusema kuwa kitendo walichofanya siyo cha kiustarabu kwani Kaseja naye ni binadamu hufanya makosa pia.
"Hakuna binadamu ambaye anafanya kazi muda wote bila kupumzika, muda ukifika Kaseja atapumzika, Kaseja ni shujaa wa taifa, wasimfanye afikirie kumaliza soka yake vibaya, kwenye klabu ambayo anaipenda, kumshutumu na kumtukana siyo jambo zuri," alisema Osiah.

0 comments:
Post a Comment