Wafanyabiashara magendo wajaribu kumuua mwanahabari
Kwa ufupi
Mpaka waandishi wa habari wanafika eneo ulipotokea
mkasa huo, tayari malori sita yalikuwa yameshavuka mpaka kupitia njia za
panya eneo la Holili kati ya saa 4:00 na saa 5:00 usiku huo.
Moshi
WAFANYABIASHARA wanaosafirisha sukari kwa magendo kwenda nchini Kenya, juzi walifanya jaribio la kumuua mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima mkoani Kilimanjaro, Charles Ndagulla.
Tukio hilo lilitokea saa 6:00 usiku, baada ya wafanyabiashara hao wakiwa na gari aina ya Toyota RAV 4J, kumgonga kwa makusudi mwandishi huyo na kufanikiwa kuvusha malori mawili yakiwa na sukari. Mwandishi wa habari hizi alishuhudia tukio hilo ambalo limeibua maswali mengi, kuhusu kiburi cha wafanyabiashara hao hadi wafikie hatua ya kutaka kutoa uhai wa mwandishi ili kutimiza malengo yao.
Kabla ya waandishi wa habari za uchunguzi kwenda eneo la Holili karibu na machimbo ya madini ya Pozorana, walidokezwa kuwa malori 12 aina ya Fusso yangevuka mpaka usiku kwenda Kenya.
Malori hayo yalikuwa yaanzie safari zake mji wa
Himo na kuelekea barabara ya Himo-Holili, kisha yangechepuka na kushika
barabara ya Lower Rombo hadi eneo hilo la madini na kuingia Kenya.
Mpaka waandishi wa habari wanafika eneo ulipotokea
mkasa huo, tayari malori sita yalikuwa yameshavuka mpaka kupitia njia
za panya eneo la Holili kati ya saa 4:00 na saa 5:00 usiku huo.
Lakini, kabla ya waandishi wa habari kwenda eneo
hilo, walimtaarifu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz
ambaye aliahidi kuwaandaa polisi kwa lengo la kukamata malori hayo.
Baada ya kufika eneo hilo, malori hayo yalijitokeza na waandishi waliyasimamisha na madereva wake kutii amri hiyo, Mwandishi wa habari hizi alimtaarifu Kamanda Boaz muda huohuo.
Pia, mwandishi wa habari hizi alimtaarifu Meneja
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro, Patience Minga
ambaye aliahidi kutuma maofisa wake wa doria.
Lakini wakati waandishi wakisubiri msaada wa
polisi, ilifika gari ndogo aina ya RAV 4J ikiwa na watu wawili mmoja
mwanamke, ambao waliwaamuru madereva hao kuondoa kwa nguvu malori hayo.
Mwandishi wa Tanzania Daima ambaye alikuwa upande wa yalipokuwa yakielekea malori hayo, aliwamulika kwa tochi watu waliokuwa katika gari ndogo ndipo walipomfuata na kumgonga.
0 comments:
Post a Comment