Baadhi ya wasafiri wa anga wanaotumia viwanja vya ndege vya Tanzania
wamelalamikia kutozwa Dola 10 ama 40 na wakati mwingine bila kupewa
stakabadhi wakisafiri nje na ndani ya nchi kupitia viwanja hivyo.
Wateja waliosafiri wiki ya mwanzo ya Septemba wakitumia ndege za Qatar Airways na Oman Air walilipigia simu gazeti hili (NIPASHE Jumapili wakihoji na kulalamikia agizo la kutakiwa kulipa Dola 40 wakiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam bila kupewa risiti wala maelezo ya kuridhisha.
Walitaka kujua sababu za tozo hilo na kuulaumu uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kwa kushindwa kuwaeleza wateja sababu za kudaiwa malipo hayo na badala yake kutakiwa kuzilipa kwenye dawati la kuhakiki nyaraka za wasafiri.
Walisema zoezi hilo lilianza mapema mwezi huu kwenye viwanja vya ndege na pale ilipoonekana wateja ni wengi walilipishwa pesa hizo bila kupewa stakabadhi licha ya kutaka wapewe nyaraka hizo.
Kufuatia malalamiko hayo NIPASHE Jumapili NIPASHE Jumapili iliwasiliana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege lakini watendaji wa ofisi hizo wakasema hawahusiki na tozo hilo na kuibebesha mzigo Mamlaka ya Kodi ya Mapato (TRA) Mkoa wa Ilala ulipo uwanja huo.
Akijibu hoja za wateja hao Meneja wa TRA wa Ilala Luvanda Ngoloka, alisema tozo hilo linatozwa wasafiri wa anga kufuatia utekelezaji wa amri ya serikali ya kuongeza kodi ya huduma za viwanja vya ndege kuanzia Julai mwaka huu. Alisema Bunge la Bajeti mwaka huu liliidhinisha tozo jipya la Dola 10 badala ya tano kwa wasafiri wa ndani na Dola 40 badala ya 30 zilizokuwa zikitozwa kabla kwa wasafiri wa kimataifa. Alisema walilazimika kutoza kodi kwa wasafiri hao wakiwa kwenye viwanja vya ndege kwa wale waliokuwa wamekata tiketi kabla ya tangazo hilo kutolewa licha ya kwamba walisafiri baada ya toza jipya kuanza kutumiwa .
Ngoloka alisema licha ya wateja kuwasilisha malalamiko yao walitoa taarifa kwa mawakala wa tiketi za ndege na kuyataarifu mashirika ya ndege yanayofanya safari nchi juu ya tozo hilo jipya.
Kuhusu wateja kukosa risiti alisema wahudumu uwanjani wanatakiwa kutoa risiti kwa wateja wanaolipa fedha hizo na kuongeza kuwa wale watakaokata tiketi kuanzia mwezi Julai tozo jipya litakuwa limeingizwa kwenye gharama za tiketi.

0 comments:
Post a Comment