,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Sunday, September 23, 2012

Ndugu zangu, 

Kwenye jamii hii tunayoishi wengi wanatumia muda mwingi kuyafuatilia maisha ya wenzao. Hivyo, wanayasahau ya kwao. Wanayakimbia maisha yao.

 Lililo jema kwa Mwanadamu ni kujitahidi kuyarudia maisha yako ili uweze kwenda mbele. Anza kwa kwa kuyatazama ya kwako. Kuna umuhimu wa kuyaishi maisha kwa uhalisia wake. Na maisha si ya asali na maziwa kila siku. Siku nyingine n i machungu kama shubili.

 Usiku huu nikiwa hapa nyumbani Iringa nimeangalia filamu ya Kiswidi nikiwa na mke na makamanda wangu. Inaitwa Anglagard- Sista gangen gylt. Inahusu maisha ya kila siku. Anglagard ina maana ya Bustani ya Malaika na Sista gangen ina maana ya mara ya mwisho. Na swali ni je, katika maisha kuna mara ya mwisho? 

Naam, na maisha nayo yanaendelea. Kesho nakwenda Tosamaganga kwenye msiba wa binti ya binamu yangu. Mjukuu wa marehemu shangazi yangu. Na huko kuna shauri nimeombwa ushauri wa namna ya kulitatua. Wajomba wa binti wa binamu wanataka maiti izikwe kijijini kwao. Na upande wetu ( kwa baba wa binti)tunaona ni mila na wajibu wetu kumzika binti yetu.

 Na kaburi limeshachimbwa. Naambiwa wajomba wa marehemu nao wameshachimba kaburi kijijini kwao. Hakuna namna yeyote ya kuigawa maiti. Busara na hekima lazima itangulizwe. Kwamba kaburi moja lazima lifukiwe bila maiti. Ni kaburi lipi? Tutajua hiyo kesho Jumapili, siku ya mazishi. 
 Alamsiki. Maggid,
 Iringa.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi