CHAUMMA waomba watengwa wa CHADEMA kujiunga na chama chao
Chama cha ukombozi wa umma(chaumma) kimefanikisha kupata usajili wa muda na bendera yake ina nembo ya ngumi, ngumi hiyo ni nembo au ishara maarufu ambayo imetumika kuwakilisha dhana na azma ya ukombozi wa watumwa katika enzi au civilization ya uyunani(Ancient Greece),na baina ya ndugu zetu wenye asili ya kiafrika kule marekani na hata katika harakati za ukombozi wa ndugu zetu Afrika kusini zilizoratibiwa na kuongozwa na chama cha ANC cha Madiba Nelson Mandela.
Nembo hio inaashiria ujasiri wa kijamii(civil courage) dhamila na azma ya kujikomboa kutoka utumwani, ugandamizwaji, upuuzwaji, unyanyaswaji, udhalilishwaji, pamoja na mateso ya ufisadi.
CHAUMMA kinapenda kuwakaribisha watu wote wa vyama vyote na wasiokuwa na vyama kujiunga na chama kipya hasa wale wanaharakati wanaotengwa chadema kwa sababu za ukabila na ukanda wanaotokea kwa sasa chama mbadala kipo.
Naamini vijana wengi wa chadema kutoka tanga, pwani, mbeya, ruvuma, lindi, mtwara, rukwa, kigoma na kanda ya ziwa wanaopigwa vita kwa sababu ya ukanda na undugu watajiunga kwa wingi sana maana hiki ni chama cha wote na sio cha ukoo flaniflani!
Tuntemeke: Jamiiforums.
0 comments:
Post a Comment