,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Sunday, July 8, 2012

Nje ya mahakama inayisikiliza kesi ya mtoto wao, mama Lulu na baba Lulu walijikuta wakiingizwa kwenye midomo ya watu waliofurika mahakamani hapo wakiwashauri waondoe tofauti zilizopita na kurudiana ili kumfanya mtoto wao, Lulu ambaye anahusishwa na kifo cha mcheza filamu Steven Kanumba kilichotokea mwezi aprili mwaka huu.


Elizabeth Michael 'Lulu'akiwa na Mama yake

Baadhi ya watu walisema katika kipindi hiki kigumu wazazi hao wa Lulu wangerudiana katika mshikamano wa maisha kitendo ambacho kingemfariji sana binti yao na kujipa moyo katika kipindi hiki cha kesi yake kusikilizwa.



“Sasa baba anaishi kivyake Arusha sijui Moshi, mama anakaa Tabata Dar si wangerudiana tu. Haya mambo yaliyompata mtoto wao yanataka ukaribu wa wazazi endapo wote wapo hai,” alisema mzee mmoja akipokuwa akizungumza na mwenzake kuhusu wazazi hao.



Wengine walimsifu mzee Michael kwa kitendo chake cha kuhudhuria siku ya kesi jijini Dar es Salaam kwani kwa mazazi mwingine angeweza kupotezea kutokana na umbali pia uchumi wan chi ambao si mzuri sana kwa miaka ya hivi karibuni.




BABA mzazi wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu'

Lakini wapo waliodai mahakamani hapo kwamba wazazi hao hawakuwahi kuishi pamoja kama mke na mume bali walikuwa wapenzi na baadaye mama Lulu akajikuta amebeba ujauzito wa mwanaume huyo.
irenemwamfupe blog

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi