,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, May 13, 2021

 

Chama Cha Mapinduzi kilifanya uzinduzi wa kampeni za ubunge katika Jimbo la Muhambwe tarehe 4 Mei 2021 na Jimbo la Buhigwe tarehe 5 Mei 2021 ukiongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Ndugu Kassim Majaliwa.Chaguzi hizi ni kutokana na kufariki kwa Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Ndg. Atashasta Nditye na Mbunge wa Buhigwe, Ndugu Philip Mpango aliyeteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ifuatayo ni tathimini fupi ya Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa marudio katika majimbo hayo ya Muhambwe na Buhigwe.

Lengo kubwa la kampeni za CCM ni kutekeleza majukumu yafuatayo;

i. Kutangaza Sera na Ilani ya CCM, kuwaeleza wananchi jinsi tulivyojipanga kuwaletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

ii. Kuwanadi kwa wananchi (wapigakura) wagombea wetu Dkt Frolence George Samizi wa Jimbo la Muhambwe na Mwalimu Eliadory Felix Kavejuru wa jimbo la Buhigwe.

Majimbo ya Buhigwe na Muhambwe ni ya CCM. Tulipoteza Mbunge wa CCM kwa kifo kule Muhambwe, hivyo wananchi wanachokitaka ni kuifariji CCM. Kwa Jimbo la Buhigwe wananchi wenyewe wanataka kumpa ahsante Mhe Rais Samia kwa kumteua Makamu wa Rais aliyekuwa mbunge wao Dkt Philip Mpango.CCM imedhihirisha kivitendo uwezo wake mkubwa wa kuwatumikia wananchi katika awamu zote za uongozi. Kazi kubwa ya kisera na utekelezaji wa miradi, kuondoa kero imefanyika  chini ya CCM kwenye majimbo ya Muhambwe na Buhigwe hivyo ushindi wa CCM ni jambo lisilo na shaka  wala wasiwasi.Mfumo wa Kampeni kwa Wagombea wetu ulijielekeza katika kufanya zaidi mikutano midogo, kukutana na kuzungumza na makundi ya kijamii katika maeneo yao/makazi/vijiji vyao.

Dkt Florence George Samizi amefika katika Kata zote 19 na amefanya mikutano midogo ya Kampeni na kukutana na makundi maalum ya Vijana, Wanawake, Wazee, Wafanyabiashara na makundi mengine ya kijamii. Wakati wote wa kampeni wananchi wamejitokeza kwa wingi kuhudhuria katika mikutano yetu ya Kampeni jimboni humo na kuonyesha matarajio yao kwa mgombea wa CCM Dkt Samizi.Ndg  Eliadory Felix Kavejuru amefanya kampeni katika Kata zote 20, na kukutana na wananchi katika Vijiji 44 sawa na asilimia 100 ya vijiji vyote na anaendelea kumalizia kampeni katika vitongoji vinane (8) vilivyobaki kati ya 192.

Mikutano mikubwa imefanywa kimkakati katika viwanja vya Shule ya Msingi Buhigwe, Munanila, na Muyama maeneo hayo yana wakazi wengi  waliojiandikisha katika kupiga  kura. Mikutano midogo 62 aliyoifanya Mgombea wa CCM Ndugu Kavejuru pamoja na mazungumzo mahsusi na makundi ya kijamii yamemkutanisha na kumpa uhakika zaidi wa kupata ushindi .Chama kimezishirikisha Jumuiya  zake zote katika kampeni za majimbo ya Muhambwe na Buhigwe pamoja na kuwatumia makada wake mbali mbali ambao wote tulia na lengo moja la kupata ushindi.Viongozo na Makada hao wamekuwa wakihutubia mikutano  ya hadhara kwa kutumia sera za chama Sera nzuri za CCM ambazo zimekuwa zikitekelezeka na kuleta manufaa kwa wananchiKampeni za CCM katika Majimbo yote mawili zitafungwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Nd. Philip Isdor Mpango tarehe 14 na 15 Mei 2021 katika uwanja wa Taifa kwa jimbo la Muhambwe na uwanja wa shule ya Mayama kwa jimbo la Buhigwe.

Tathmini ya awali imeonesha katika majimbo hayo CCM itashinda si chini ya 80% na ikumbukwe ushindi huu hautakuwa mgeni kwetu kwani CCM ni kinara na baba wa mageuzi ya demokrasia ya nchini, Afrika Mashariki na Kati.

Nilisema Siku ya uzinduzi na ninaendelea kusisitiza CCM itashinda Buhingwe na Muhambwe  kwa haki, amani na utulivu mkubwa pamoja na yote lakini ya sababu kubwa za ushindi ni imani kubwa walionayo wananchi kwa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Chama Cha Mapinduzi.

Chini ya Uenyekiti wa CCM wa ndugu Samia Suluhu Hassan tutaendelea kuvilea vyama vya siasa chini ili viendelee kufanya siasa safi na yenye tija kwa Taifa baada ya kufanya siasa za danadana. Sote tunajenga nyumba moja hakuna sababu kugombeana fito.Ikumbukwe kuwa tokea siasa za nchi hii kuanzia TANU hatimae CCM Chama chetu hakijawahi kufanya makosa katika mambo ya msingi yanayohusu maslahi ya Taifa tunakumbusha kuwa uchaguzi wa Buhingwe na Muhambwe umebeba maslahi mapana ya Taifa kwa maana unakwenda kuzalisha wabunge wanakwenda kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo endelevu ya kiuchumi, kijamii na kisiasa hivyo hatuwezi kufanya makosa.

Tumejipanga kuhakikisha Wanachama wetu waliojiandikisha wanajitokeza kwa wingi katika vituo vya kupigia kura na kuwachagua Wabunge wanaotokana na Chama chao pendwa.

Aidha tunatoa wito kwa vyama vingine na wananchi kwa ujumla kuendelea kudumisha  amani, usalama na utulivu ambao umekuwepo  wakati wote wa kampeni zetu.

Thursday, April 8, 2021


Waziri ataka waalimu kuchangamkia FURSA. Sekta ya benki imepiga hatua kubwa sana Nchini Tanzania kwenye miaka ya 2000. Umuhimu wa sekta hii ndio ulimpelekea Waziri Suleiman Jafo kuwataka waalimu Nchini Tanzania kuchangamkia FURSA ya mikopo na huduma ya benki yao ya Mwalimu commercial bank ambayo sasa inawawezesha kupata huduma kupitia matawi, ATM, Mwalimu Wakala na Mwalimu mobile popote Tanzania. Akizungumza wakati wa kuzindua huduma ya Mwalimu Visa Card Waziri Jafo alisema kwa waalimu ambao wanalenga kujikomboa kiuchumi ni vizuri wakatumia huduma za Mwalimu bank kwani sio tu inawapa mikopo nafuu lakini pia inawajali kabla ya ajira na baada ya ajira yaani wakistaafu.

Thursday, February 4, 2021


Katika kuelekea sikukuu ya Valentine Day (SikuyaWapendanao) watu mbalimbali wamekuwa na kawaida ya kuitumia siku hii kufurahia na wapendwa wao kwa kuwa nao karibu na kuwapatia zawadi mbalimbali kama sehemu ya kuonesha umuhimu na jinsi wanavyowajali wapendwa wao. Leo tarehe 04/02/2021 katika ukumbi wa Mikutano wa Maendeleo Bank iliyopo Posta jijini Dar es Salaam, Meneja wahuduma kwaWateja wa Maendeleo Bank Sylvia Chaula, amezindua rasmi kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO itakayoanza siku ya leo tarehe 04/02/2021 hadi tarehe 13/02/2021 ikihamasisha wateja wote wa Maendeleo Bank kutumia huduma ya MB Mobile (*150*52#) pamoja na huduma za mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao za Maendeleo Bank.

Sylvia Chaula ameeleza kuwa kilele cha kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO kitakuwa ni siku ya wapendanao (Valentine’s day) yaani tarehe 14/02/2021 ambapo washindi watatu watakaoshinda watapata zawadi mbalimbali kama vile Laptop, Simu Janja, Saa pamoja na kupata chakula cha usiku naMkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Dr Ibrahim Mwangalaba pamojana jopo la wafanyakazi wa Maendeleo Bank katika Hotel ya Holiday Inn iliyopo Posta. Washindi wote watatu watapata nafasi adhimu ya kuwaalika wapendwa wao katika chakula cha usiku, yaani kila mshindi atakujana +plus one wake katika siku hiyo ambapo pamoja na chakula cha usiku pia kutakuwa na tukio la washindi kupokea zawadi zao kutoka Maendeleo Bank. Aliongeza Sylvia Chaula. Unajua maneno matupu hayanogeshi shughuli, siku hiyo ya wapendanao sisi kama Maendeleo Bank tunapenda kutumia muda wetu kuwaonyesha wateja wetu kuwa tunawapenda, tunawajali na kuwathamii ndio mana tumechagua siku hiyo kuwaonyesha wateja wetu upendo tulionao kwao kwa vitendo na sio maneno.
  Aliongeza Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Bank na Tehama Ndg. George Wandwalo. Katika kudumisha ushirikiano na upendo uliopo baina ya Maendeleo Bank na wateja wake, Maendeleo Bank kupitia Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa benki Ndg. Wandwalo alitoa zawadi mbalimbali kwa wanahabari waliofika kwenye mkutano wa leo kama sehemu ya kuanza rasmi kwa kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO.

Tuesday, December 8, 2020


Mahafali ya Tatu ya huo ha Urembo cha Manjano Beauty academy mwaka 2020 Yamefanyika Ambapo Wahitimu wa Chuo cha Urembo cha Manjano wametunikiwa vyeti katika nyanja ya urembo na vipodozi (Cosmetology).

Mkuu wa Chuo cha Urembo Mama Shekha Nasser akizungumza machache wakati wa mahafali ya Tatu ya Chuo cha Manjano Beauty Academy. Amewataka wanawake kujiongezea elimu ya matumizi sahihi ya Vipodozi na Urembo ili kuweza kutoa huduma sahihi na yenye ueledi kwa wananchi. Mama Shekha alisema Tanzania kuna upungufu mkubwa wa Wataalamu, hasa walimu wenye sifa za kufundisha elimu ya Urembo na Vipodozi, hivyo aliwashauri wanawake wengi kujiunga na Chuo cha Manjano Beauty Academy ili waendeleze tasnia hii na kuboresha huduma zao kwa wateja. Aidha alitaja changamoto kubwa alizokabiliana nazo wakati anaanzishi Chuo hicho ikiwemo ukosefu wa wataalamu wazawa wa maswala ya Urembo na Vipodozi. Akieleza zaidi alisema sekta ya urembo ina fursa kubwa kwa ajira na inaweza kusaidia kujiongezea kipato na kuondokana na ukosefu wa ajira na umasikini.

Mgeni rasmi, uongozi wa Chuo cha Manjano Bauty Academy na Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja.

Mgeni Naye Aliwapongeza wanawake wa Kitanzania waliojiunga kwenye chuo hicho kwa lengo la kupata ujuzi wa maswala ya urembo na vipodozi. Alisema Urembo, Vipodozi na mitindo ni moja kati ya sekta zinazoajiri mamilioni ya wanawake kwa sasa, na kuchangia kwa kiasi kwenye pato la Taifa. Akiendelea zaidi alisema, elimu na mafunzo kwa vitendo (Vocational training) ni elimu na mafunzo ambayo yanayotoa ujuzi na elimu muhimu kwa ajili ya ajira. Elimu ya aina hii ni ambayo humuandaa mtu kufanya kazi katika fani mbalimbali, kama biashara, utengenezaji wa vitu, au kama fundi. Hivyo aliwausia wahitimu kuitumia vizuri elimu na ujuzi walioupata kwenye Chuo cha Manjano. Alielezea pia kwa kusema elimu ya ufundi na ujuzi ni muhimu katika kuleta usawa kwenye jamii kwani ni moja ya kitovu cha kuleta maendeleo na kuendana na kasi ya Awamu ya Tano ya Uchumi wa Viwanda. 





Tuesday, October 6, 2020

Monday, October 5, 2020

Wednesday, September 30, 2020

Monday, September 28, 2020

Sunday, September 27, 2020

Wednesday, September 23, 2020

Thursday, September 17, 2020

Tuesday, September 15, 2020

Friday, September 11, 2020

Thursday, September 10, 2020

Saturday, September 5, 2020

Thursday, September 3, 2020

Friday, August 28, 2020

Tuesday, August 25, 2020

Thursday, August 20, 2020

Wednesday, August 19, 2020

Monday, August 17, 2020

ufunguzi